Maandamano nchini Argentina

Maelfu ya raia  nchini Argentiwa waingia mabarabarani kuandamana kupiga kupanda kwa bei za bidhaa mahitaji

Maandamano nchini Argentina


Maelfu ya raia  nchini Argentiwa waingia mabarabarani kuandamana kupiga kupanda kwa bei za bidhaa mahitaji  nchini humo.
Waandamanaji  wamekemea kupanda kwa bei za umeme , maji na gesi wakitolea wito serikali kupunguza bei na kuongeza mishahara.
 Buenos Aires, mashirika ya wafanyakazi na vyama vya kisiasa  pamoja na mashirika yasiokuwa ya kiserikali yalitolea wito  maandamano   kwa şengo la kupinga  kupanda kwa bei za  bidhaa mahitaji huku mishahara ikiwa ya kiwango cha  chini.
Katika maandamano hayo, waandamanai wamekemea uongozi wa rais  Mauricio Macri na serikali yake.

Maeflu ya waandamanaji  walikutana katika kitongoji cha May na kujielekeza katika jengo la bunge kuonesha ghadhabu zao dhidi ya serikali kwa kupandisha bei za umeme na gesi  huku mishahara ikiwa ya kiwango cha chini.
Mashirika yaliotolea wito maandamano hayo, uongozi wake umefahamisha kuwa  maandamano hayo yataendelea mjini Buenos Aires,  Cordoba na Comodoro Rivadavia.
Jeshi la Polisi limefunga baadhi ya barabara kuzuia ghasia huku  shughuli za uchukuzi zikisitishwa katika miji tofauti.

Kulingana na taarifa zilizotolewa na viongozi waliotoa wito wa  maandamano, maandamano hayo yataendelea hadi Februari 7.Habari Zinazohusiana