Iran kurusha sateliti 2 angani wiki ijayo

Rais wa Iran Hasna Ruhani amesema wiki inayokuja Iran itarusha sateliti 2 angani

Iran kurusha sateliti 2 angani wiki ijayo

 

Rais wa Iran Hasan Ruhani amesema wiki ijayo Irani itarusha kuelekea anga la mbali sateliti mbili. 

Ruhani pamoja na viongozi wa kisiasa na dini walihudhuria katika maadhimisho ya miaka 2 ya kifo cha rais wa zamani wa taifa hilo Ali Akbar Hashimi Rafsanjani. Maadhimisho hayo yalifanyika mji mkuu wa nchi hiyo Tehran.

Katika hotuba yake aliyoitoa katika maadhimisho hayo Ruhani, alisema kwamba nguvu za kiulinzi  pamoja na teknolojia mpya na ya kisasa ilizokuwa nazo Iran hivi sasa ni juhudi za kazi za Rafsanjani, akaongeza kwamba wikiinayofuata Iran itarusha angani sateliti 2.

Hasan Ruhani,alisema kwamba  Rafsanjani ni mwanasiasa wa kipekee hakuna mfano wake.

Rais wa zamani Hashimi Rafsanjani,alifariki katika bwawa la kuogolea mnamo tarehe 8 Januari 2017.

 


Tagi: Iran

Habari Zinazohusiana