Donald Trump kutohudhuria Jukwaa la kiuchumi la Davos

Rais wa Marekani kutohudhuria jukwaa la kiuchumi la dunia linalofanyika Davos Kutokana na mgogoro wa muda wa kibajeti unaoendelea nchini Marekani

Donald Trump kutohudhuria Jukwaa la kiuchumi la Davos

 

Rais wa Marekani Donald Trump, kutohudhuria jukwaa la uchumi la kidunia linalofanyika kijiji cha Davos nchini Uswizi. Hiyo ni kutokana na changamoto ya muda ya bajeti iliyopelekea baadhi ya idara za serikali kufungwa. 

Katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii Twitter rais Trump ameandika kwamba kutokana na kutofikia makubaliano na wanademokrat kuhusiana na suala la ulinzi wa mpakani pamoja na ulinzi wa kitaifa , kwa heshima zote ameifuta safari yake ya Davos alikokuwa aende kushiriki jukwaa la kiuchumi la dunia.

 


Tagi: Trump , Davos

Habari Zinazohusiana