Balozi mdogo wa Irak mjini Mashhad arejeshwa nyumbani

Irak yamrejesha nyumbani balozi wake mdogo wa mjini Mashhad kwa kushiriki katika tangazo la biashara

Balozi mdogo wa Irak mjini Mashhad arejeshwa nyumbani

 

Balozi mdogo wa Irak mjini Mashhad nchini Iran, Yasin Sherif arudishwa nyumbani kutokana na kushiriki katika tangazo la Hospitali ya huduma ya upasuaji wa kubadili maumbile na baadaye tangazo hilo kuenezwa kupitia mitandao ya kijamii.

Katika taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje ya Irak inasema Waziri wa mambo ya nje wa Irak Muhammed Hakim, amemrudisha  Baghdad balozi mdogo wa Mashhad kutokana na tangazo lilimuonyesha balozi huyo  akiitangaza hospitali ambalo lilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Katika tangazo hilo balozi huyo anaonekana akiitambaulisha hospitali hio akisema inatoa huduma za upasuaji wa kubadili maumbile, kupandikiza nywele, na huduma za meno kwa bei nafuu.


Tagi: Iran , Irak

Habari Zinazohusiana