Tajiri namba 1 duniani kutalikiana na mkewe

Jeff Bezos ambaye kwamujibu wa jarida la Forbes ndiye tajiri namba moja duniani hvi sasa ametangaza kutalikiana na mkewe

Tajiri namba 1 duniani kutalikiana na mkewe

 

Bilionea mkubwa duniani na mkurugenzi mkuu wa Amazon, shirika kubwa la biashara ya kimtandao, Jeff Bezos pamoja na mkewe MacKenzie Bezos wametangaza wataivunja ndoa yao iliyodumu kwa muda wa miaka 25. 

Mkurugenzi mkuu na mwanzilishi wa shirika lenye makao yake makuu nchini Marekani Jeff Bezos na mkewe MacKenzie Bezos, wamefikia uamuzi wa kutalikiana na hivyo kuhitimisha ndoa yao iliyodumu kwa muda wa miaka 25.
Bezos, 54, ambaye kwa mujibu wa jarida la Forbes ndiye tajiri namba moja duniani na mkewe MacKenzie Bezos ,48, wametangaza habari ya kutalikiana kwao kupitia ukurasa wa mtandao wa jamii wa Twitter wanaoutumia pamoja.

Katika ujumbe huo iliandikwa, Wamechukua uamazi wa kutalikiana, hilo limekuja baada ya kujaribu kutengana. wataendelea kubaki kama marafiki na kwamba kukutana kwao ilikuwa ni bahati kubwa, na wanashukuru sana kwa kila mwaka walioishi pamoja katika ndoa. Na kwamba hata kwamba wangefahamu kwamba ndoa yao ingemaliza kwa talaka baada ya miaka 25, bado wangeoana vilevile.
Bezos walifunga pingu za maisha mnamo mwaka 1993 na katika mahusiano yao wamebarikiwa kupata watoto 4.
Kwa mujibu wa jarida la Forbes la mwezi Oktoba ana ukwasi wa dola bilioni 160 na hilo limemfanya tajiri namba moja duniani.

 Habari Zinazohusiana