MERWE WA YEMEN

Upembuzi huu umefanywa na Prof. Dr. Kudret BÜLBÜL mkuu wa kitivo cha elimu ya siasa chuo kikuu cha Ankara Yıldırım Beyazıt

MERWE WA YEMEN

Mara nyingine huwa tunakuza sana matatizo madogo tuliyonayo ... Tunaweza kufanya maisha yawe magumu sana kwetu sisi wenyewe,kwa mazingira yetu na kwa nchi yetu, kama tutaangalia kutokea ndani. Katika mazingira kama hayo inafaa zaidi tukitoka nje na kuitazama nchi kutokea nje. Kuangalia matatizo ya nchi kwa jicho la kutokea nje ya nchi kunaweza kusaidia kufanya tathmini sahihi zaidi. Kwa munasaba huo nitatumia simulizi ya kweli kuelezea mtazamo wangu juu ya maana ya hilo kwa Uturuki.  

Pamoja na kwamba Uturuki inapitia hali ya kipekee, kadiri siku zinavyozidi kwenda Uturuki inakuwa kitovu cha elimu. Kipindi nikiwa mwanafunzi Uturuki  haikuwa nchi ambayo watu huenda katika kutafuta maisha yao ya baadaye lakini hivi sasa Uturuki kuna wanafunzi wa kimataifa wanaokaribia 150 elfu.Wanafunzi hawa wapo katika kutafuta maisha yao ya baadae. Kwa haraka haraka tunaweza kusema namba tuliyoitaja ni kiwakilishi tu. Inawakilisha hadithi tofauti, ambapo maisha ya kila mmoja wao  ni hadithi tofauti, juhudi tofauti, machungu tofauti, matumaini tofauti na mategemeo tofauti. Kwa wanafunzi hawa ni jishi gani Uturuki ina maana kwao au inawaletea hisia gani.Katika kujadili hili nitatumia hadithi ya Merwe mwanafunzi kutoka Yemen.

Prof. Dr. Kudret BÜLBÜL mkuu wa kitivo cha elimu ya siasa chuo kikuu cha Ankara Yıldırım Beyazıt anajadili mada hii..

Mama yangu ni Yemen, Uwaridi ni magugu..

Yemen… nchi inayopakana na pwani ya bahari ya shamu, ghuba ya Adeni na pwani ya bahari ya Oman. Eneo la kijiografia inapopatikana nchi hio ni eneo la kimkakati, kutokana na hilo  karibu katika vipindi vyote vya kihistoria nchi hii  imejikuta katika matatizo na maumivu mengi.  Kwa mtazamo wa Uturuki ukiachilia mbali askari iliowapoteza katika ulinzi wa Makka na Madina Yemen inakuwa ni moja ya maeneo ambayo wanajeshi wengi wa Uturuki wamemwaga damu. Yemen pamoja na Çanakkale ni katika maeneo yaliyoleta huzuni nyingi, ni katika maeneo ambayo moyo wa Uturuki ulitikisika. Yemen ni nchi ambayo ilisababisha mabinti wadogo wa kituruki wenye umri mdogo wa miaka 15 kumwaga machozi.  Yemen kama ilivyo kwa Çanakkale ni nchi ambayo imeshuhudia machungu mengi, majonzi makubwa. Ukizingatia na idadi ya askari wa kituruki waliopoteza maisha katika kuitetea nchi hiyo, kwa maneno mengine unaweza kusema Çanakkale na Yemen ni maeneo yenye kumbukumbu ya majonzi kwa taifa la Uturuki.

Safari ya Matumaini...

Merwe anatokea San’a mji mkuu waYemen.  Kama ilivyo kwa vijana wote wanapokuwa wakitafuta maisha,  Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoigubika nchi hiyo mnamo mwaka 2014 vilizima ndoto za kijana huyo. Kipindi cha mapinduzi ni silaha pekee ndio zilizokuwa zikiongea, Utu ulisahaulika, vijana na hata mustakabali wa taifa pia vilisahaulika..

Mwaka 2015 akiwa katika hali ya mfazaiko huku akiwa hajui nini cha kufanya kuhusiana na mustakabali wake kutokana na machafuko yaliyotanda nchi nzima kipindi hicho. Merwe anapata  tumaini jipya baada ya kupokea taarifa kwamba amepata nafasi ya masomo nchini Uturuki kwa udhamini wa YTB. Kipindi hicho taasisi zingine kama Fulbright ya Marekani, Daad ya Ujerumani na Chevening ya Uingereza zilikuwa zimesitisha kutoa udhamini kwa wanafunzi kutoka Yemen kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe, hivyo basi udhamini wa YTB kwa Merwe na wanafunzi wengine 150 kutoka Yemen ndio ulikuwa mwanga na tumaini pekee lililobaki. Vijana hawa wakiwa na ndoto za Uturuki, Kwenda Uturuki kisha baadae warudi kuijenga upya nchi yao iliyoharibiwa na vita, walikuwa na msisimko wa kipekee.

Kwa upande mmoja kuna tumaini lakini upande mwingine ni ukweli ulio mchungu. Kutokana na vita hivyo ofisi za balozi zilizokuwa San’a  zilikuwa zimefungwa , Ofisi nyingi zilihamishiwa Jidda. Safari za ndege nazo zilisimamishwa kwa sababu za kiusalama. Ili aweze kuja Uturuki alihitaji viza. Na kwa ajili hiyo ilimlazimu afunge safari kwa njia ya barabara kwenda Jidda ambako ofisi za ubalozi wa Uturuki zilikuwa zimehamishiwa. Lakini makundi tofauti yalikuwa yakipigana yalikuwa yametapakaa eneo lote hilo la barabara ambayo angepita, mapigano, mashambulizi vituo vya kukaguliwa na mambo mengine kama hayo viliifanya safari yake ya kuufikia mpaka wa Saudia iwe kama haiwezekani. Na hata kama akifika mpakani hakuwa na uhakika kama angeruhusiwa kuingia Saudia.

Vijana ambao hawakuwa na namna katika kutafuta suluhisho walikusanyika pamoja mjini San’a wakawasiliana na ubalozi wa Ututuki uliokuwa Jidda. Wakaambiwa inabidi wazipeleke hati zao za kusafiria Jidda kwa ajili ya viza, zaidi ya hapo hakuna suluhisho jingine. Mwishoni ikaamuliwa kwamba mwanafunzi mmoja wa kiume ajitolee kupeleka hati za wanafunzi wote Jidda.Vijana wakiwa na matumaini makubwa wakaanza kuzikusanya hatiza kusafiria za wanafunzi wote waliochaguliwa nchi nzima.Lakini matumaini yao hayakudumu kwa muda mrefu.Kijana wa kiume ambaye angejitolea kuzipeleka pasi za kusafiria Jidda hakupatikana, hilo linatokana na ukweli kwamba safari ya Jidda ilimaanisha kukatisha miji yote ya Yemen ambayo ilikuwa chini ya mvua za mabomu, hakukuwa na mwenye ujasiri, hilo lilikatisha tamaa. Wakiwa katika hali ya kupoteza kabisa matumaini “ Ilipoulizwa nani atajitolea, bila kuangalia kushoto wala kulia,  mimi hapa”

Merwe kwa utambuzi akajitolea kuchukua hati zote za kusafiria zilizokusanywa kuzipeleka Jidda.Uamuzi wa Merwe ulisababisha wasiwasi mkubwa kwa familia yake, wakajaribu kumshawishi aachane na maamuzi hayo. Na hata kama atakwenda basi apeleke hati yake peke yake  ili kupunguza uwezekano wa hatari. Lakini Merwe  alishikilia msimamo wake akifahamu kwamba wanafunzi wote walioshinda nafasi hizo za masomo walikuwa wakimtegemea  yeye. Kwa haraka haraka wakafanikiwa kukusanya hati za wanafunzi 90. Baadhi ya wanafunzi hawakupatikana na wengine kwa kuzani kwamba hatoweza kufanikiwa hio safari na hata akifanikwa asingeruhusiwa kuingia Saudia na lundo la paspot, hawakuwasilisha paspoti zao. Balozi we Uturuki kipindi hicho, Fazlı Çorman, alifurahishwa sana na uamuzi wa  Merwe. Lakini alirudia mara kumi kumi kumuelezea hatari ya uamuzi alioufanya. Alimwambia ikitokea amekamatwa na paspot nyingi kiasi hicho inawezekana akaingia matatizoni kupelekea kuyaweka maisha yake hatarini. Lakini pamoja na yote hayo alimwambia kwamba angeweza kumpatia barua inayoonyesha kwamba amepatiwa udhamini wa masomo Uturuki, hivyo anapeleka hati yake pamoja na za vijana wengine waliopata nafasi hiyo kwa ajili ya mchakato wa kupatiwa viza.

Familia ya Merwe na Wanafunzi wengine wakaomba dua kisha Merwe  akaanza safari yake iliyodumu kwa siku mbili moja kwa moja mpaka katika mpaka wa Saudia. Labda kutokana na dua zilizoombwa merwe angefika salama bila kukumbwa na dhahama yeyote. Kutokana na utamaduni wa Yemen pamoja na kuwapo kwa vituo vingi vya ukaguzi, kutokana na kuwa ni mwanafunzi wa kike  hakufanyiwa upekuzi wa kina. İlipofika mida ya saa 4 asubuhi akawafikia maafisa wa uhamiaji wa Yemen. Lakini mbele yake kulikuwa na msururu mkubwa wa watu. Kutokana na msururu huo haikuwa rahisi kwa yeye kupata nafasi siku hiyo kama angesubiria, Hivyo kwa namna moja au nyingine  baada ya kuongea na askari hao wa Yemen aliruhusiwa kupita. Akaanza kutembea kuelekea kwa askari wa uhamiaji upande wa Saudia mgongoni akiwa na begi lenye paspoti 90 za wanafunzi.

“Maharimu” Huwezi kuingia ..

Maafisa uhamiaji wa Saudia hawakukubali kirahisi, Maafisa hao hawakumuamini Merwe. Huku akiwa amekasirika maafisa wale walimwambia hakuna wanachoweza kufanya kwa siku hiyo, aondoke arudi siku inayofuatia. Katikati ya jangwa mtoto wa kike peke yake atafanya nini ? Merwe ikabidi afanye tena mawasiliano na ubalozi. Ubalozi ukatuma faksi inayoelezea suala zima. Maafisa wa uhamiaji safari hii wakamwambia kwamba hawawezi kumruhusu kupita kuingia Saudia bila kuwa na maharimu (mume,baba, kaka n.k) aliyeambatana naye. Merwe hakwenda Saudia kuhiji, Asingekaa zaidi ya siku tatu baada ya mchakato wa viza angengeuza mara moja, alirudia maneno hayo kuwaelezea maafisa wale, Hata baada ya kufanikiwa kuwashawishi maafisa wale ilibidi waandike jina rasmi la maharimu wa Merwe, Baada ya masaa 9 walimruhusu kupita.

Maafisa wa ubalozi walimpokea Merwe kwa furaha na bashasha kubwa. Ndani ya siku tatu walifanya kazi kwa bidii wakafanikisha mchakato wa viza. Lakini kwa Merwe ugumu haukuwa umeisha njia ya kurudi ilikuwa na hatari vilevile kama wakati wa kuja. Wakati akirejea akiwa ndani ya basi katika daraja moja walinusirika kwa dakika chache mno kulipuliwa na bomu. Basi hilo baada ya safari ya muda jangwani na kusimamishwa mara kwa mara sehemu za ukaguzi mwishowe liliwasili tena San'a.

Merwe sasa hivi ni mwanafunzi wangu katika chuo kikuu cha Yıldırım Beyazıt, yeye pamoja na wanafunzi wenzake wanaendelea vizuri na masomo yao tena  kwa juhudi kubwa ili waje kuijenga tena nchi yao.

Simulizi hii iwafikie wale wote wanaosema haiwezekani tena kuishi Uturuki, naodoka huku wakitoa kila aina ya upinzani na mara nyingine wakitukana kwa kukosa adabu, Hata kama wanastahiki kupata zaidi, simulizi hii iwafanye watafakari na kujitathmini upya hata kama ni kwa kiasi kidogo. 

Ufafanuzi wa Prof. Dr. Kudret BÜLBÜL mkuu wa kitivo cha elimu ya siasa chuo kikuu cha Ankara Yıldırım Beyazıt 

 

                                                                 

                                                           


Tagi: Merwe

Habari Zinazohusiana