Mpango wa Trump " Makubaliano ya Karne" waaihirishwa

Mpango wa Donald Trump wa kuleta amani mashariki ya kati unaojulikana kama "Makubaliona ya karne" umeaihirishwa

Mpango wa Trump " Makubaliano ya Karne" waaihirishwa

 

Balozi wa Marekani nchini Israel David Friedman, amesema "makubaliano ya karne" yaliyokuwa yatangazwe na rais Donald Trump yamehairishwa. Makubaliano hayo lengo lake ilikuwa ni kuleta amani mashariki ya kati.

Friedman alihuzuria katika kikao na waandishi wa habari kilichoandaliwa kwa ajili ya mshauri wa masuala ya usalama wa taifa wa rais Trump, John Bolton, ambaye yupo ziarani nchini Israel.

Friedman alisema Trump amehairisha mpango wa amani baina ya Palestina na Israel kwa miezi kazaa.

Moja ya sababu za kuhairishwa kwa mpango huo ni kutokana na kukaribia kwa tarehe za uchaguzi mkuu nchini Israel, na nyingine ni kutokana na uongozi wa Palestina kuupinga mpango huo wa Marekani.

 

 Habari Zinazohusiana