Iran yapiga marufuku matangazo ya biashara ya bidhaa za kigeni

Bunge la Iran limetisha sheria inayopiga marufuku matangazo ya biashara ya bidhaa zinazozalishwa nje ya nchi hio

Iran yapiga marufuku matangazo ya biashara ya bidhaa za kigeni

 

Nchi ya Iran imepiga marufuku matangazo ya biashara ya bidhaa zinazo zalishwa nje ya nchi hio. Hilo ni katika kuunga mkono biashara ya bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na kituo cha habari rasmi cha bunge la nchi hio, zinasema bunge la nchi hio limepitisha kanuni ya 19 ya sheria ambayo inapiga marufuku matangazo ya biashara ya bidhaa zote za mataifa mengine ambazo pia zinazalishwa nchini humo. Sheria hiyo inapiga marufuku matangazo ya biashara ya kwenye televisheni, redio, magazeti, mabango na aina zote za vyombo vya matangazo.

Sheria hio haikulenga bidhaa ambazo umaliziwaji wake hufanyika nchini Irani, imelenga bidhaa ambazo hutengenezwa kwa asilimia mia kwa mia katika nchi nyingine. Kwa mujibu wa sheria hiyo yeyote atakayekiuka sheria hiyo atapatiwa adhabu kali.

 


Tagi: Iran

Habari Zinazohusiana