Leo Katika Historia

Picha ya kwanza kupigwa duniani iliwasilishwa na mmoja wa wagunduzi wake tarehe 2 Januari

Leo Katika Historia

 

Ingawa   tarehe rasmi ambayo picha ya kwanza duniani ilipigwa haifahamiki , kwa mara ya kwanza picha hiyo iliwasilishwa na mmoja kati ya wagunduzi wake,mpiga picha wa kifaransa Louis Daguerre  mwaka  1839. 

******

Mnamo mwaka 1905 katika vita vya Urusi na Japan, Ngome ya Urusi iliyokuwa China iliyojulikana kama  Port Arthur, ilijisalimisha kwa kikosi cha jeshi la maji la Japan kilichokuwa chini ya admirali Heihachiro Togo. Huo ndio ulikuwa mwanzo wa kushindwa na hatimaye  kupelekea mapinduzi ya mwaka 1905 pamoja na kuvunjika kwa dola la kirusi.

******

Utaratibu uliokuwa ukitumika nchini Uturuki kuwatambua watu kwa kuwaongezea jina katika majina yao lililokuwa likionyesha dini, jamii na cheo cha kifamilia, ulifanyiwa mabadiliko rasmi ya kisheria  tarehe 21 Juni 1934 kisha kutambulishwa sheria ya jina la ukoo,sheria ambayo iliweka ulazima kila mtu kuwa na jina la ukoo la kituruki. Sheria hio ilianza kutumika Tarehe 2 Januari mwaka 1936.

******

Mnamo mwaka 1959 chombo cha kwanza kufika katika mipaka ya mwezi na kuingia katika obit za sayari za jua kilichojulikana kama “Luna1”  kilirushwa kuelekea angani na jamuhuri ya kisoviet (USSR). Luna 1 ilikuwa ni ndoto, na ni chombo “satelite” cha kwanza cha anga za mbali kuzunguka jua katika obit za sayari.

******

Mnamo mwaka 1975 redio ya Uturuki ilianza kurusha matangazo kama idhaa tatu tofauti kwa majina ya  TRT1, TRT2 na TRT3

******

Mnamo mwaka 1979  baada ya juhudi za pamoja za miaka mitano za wana archelojia wa kituruki na wa kimarekani merikebu ya kwanza ya kiislamu kuzama duniani ilipatikana katika bahari ya Aegean.

******

Mnamo mwaka 1993 Jeshi la Uturuki kwa mara ya pili lajielekeza nje ya mipaka yake  katika oparesheni nchini Somalia baada ya ombi la Umoja wa mataifa. Mara ya kwanza jeshi la Uturuki kufanya oparesheni nje ya mipaka yake ilkuwa miaka 43 kabla ya hapo, oparesheni iliotekelezwa nchini Korea. Somalia ilikuwa imekumbwa na janga la vita ya wenyewe kwa wenyewe pamoja na baa la njaa.


Tagi: Historia

Habari Zinazohusiana