Evo Morales ruksa kugombea muhula wa nne wa urais

Mahakama kuu nchini Bolivia yamruhusu rais wa nchi hio Evo Morales kugombea urais kwa mara ya 4

Evo Morales ruksa kugombea muhula wa nne wa urais

 

Mahakama kuu ya uchaguzi nchini Bolivia imeruhusu rais wa nchi hiyo Evo Morales aweze kuwa mgombea kwa mara ya nne katika uchaguzi mkuu utaofanyika mwaka 2019.

Rais wa mahakama hiyo Maria Eugenia Choque, amesema Morales anaweza kugombea tena aongoze kwa muhula wa nne. Choque ambaye hakutaka kujibu swali lolote la wanahabari alisema kwamba wamefikia uamuzi, Morales anaweza kugombe katika uchaguzi wa mwaka 2019.

Wakati wafuasi wa Morales wakisherehekea maamuzi hayo ya mahakama karibu na ikulu ya nchi hio, Wapinzani katika kupinga maamuzi hayo wameingia mitaani kuandamana nchi nzima kwa ujumla.

Morales alishinda uchaguzi mkuu wa rais uliofanyika Decemba 18 2005 na kukalia kiti cha uraisi.

Katiba ya Bolivia inaruhusu mtu mmoja kukalia kiti cha urais mfululizo kwa mihula miwili. Kutokana na kwamba kipindi cha miaka 5 kilikuwa hakijatimia Morales aliweza kuwania urais kwa muhula wa tatu mwaka 2014. Mwaka 2016 waliitisha kura ya maoni kubadilisha katiba ili Morales aweze kugombea kwa muhula wa nne. Ambapo asilimia 53.91 walisema hapana.

Mahakama ya katiba ilifungua shauri kuhusiana na uwezekano wa Morales kuwa mgombe kwa muhula wa nne mwaka 2019

Taarifa iliyotolewa na mahakama ni kwamba katazo linalomnyima haki Morales ya kugombea muhula wa nne wa urais halina mashiko. Na kwamba kura ya maoni waliosema hapana walishinda kwa kiwango kidogo.

 Habari Zinazohusiana