Jeffrey kuzuru Ankara leo kwa ziara ya kikazi

Mwakilishi wa Marekani kwa Syria James Jeffrey kuzuru mjini Ankara kwa ziara ya kikazi

Jeffrey kuzuru Ankara leo kwa ziara ya kikazi

Mwakilishi maalumu wa Marekani kwa Syria James Jeffrey, kuzuru Ankara leo.

Mwakilishi huyo ambaye atazuru Jordan mnamo Decemba 14, anakuja kwa ajili ya suala la Syria.

Katika taarifa iliyotolewa na waziri wa mambo ya nje wa Marekani inasema Jefrey atazuru Uturuki na Jordan na ataambatana na katibu msaidizi wa wizara hiyo Joel Rayburn.

Jefrey pamoja na viongozi atakaokutana nao nchini Uturuki watazungumzia kuhusu hali ilvyo hivi sasa nchini Syria kisha wanataraji kuunda kikosi kazi cha ngazi ya juu cha Syria.

Nchini Jordan James Jefrey anatarajiwa kujadili namna ya kuuwekea vikwazo vikali zaidi utawala wa Syria, Uamuzi namba 2254 wa baraza la usalama la Umoja wa mataifa kuhusiana na suluhisho la kisiasa na hatua  za kufuata pia zitajadiliwa 

Jeffrey akiwa ankara  atakutana pia na wanadiplomasia wa Marekani waliopewa kazi ya kutengeneza sera za syria.

 Habari Zinazohusiana