Ethiopia yaisihi Yemen kuachana na vita

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ameitaka Yemen ifanye mazungumzo kwa ajili ya kurudisha amani nchini humo.

Ethiopia yaisihi Yemen kuachana na vita

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ameitaka Yemen ifanye mazungumzo kwa ajili ya kurudisha amani nchini humo.

Ahmed ameitaka Yemen kujaribu kurudisha amani bila ya umwagaji damu wa aina yoyote.

"Fanyeni mpango wa kuikuza na kuiendeleza nchi yenu kama ilivyokuwa hapo awali",alisema waziri huyo.

Waziri huyo aliongeza kwa kusema kuwa vita haitowaletea manufaa yoyote wananchi wa Yemen bali ndo kwanza inazidi kuiangamiza nchi.

Yemen imekuwa katika vita toka mwaka 2014 baada  ya kundi la Houthi kutawala sehemu kubwa ya nchi hiyo.Hali ilizidi kuwa mbaya mwaka 2015 baada ya  Saudi Arabia kuingilia kati.

Umoja wa Mataifa umetoa ripoti inayoonyesha kuwa kuna hatari kubwa ya mamilioni ya wananchi wa Yemen kupatwa na janga la njaa huku maelfu wakiwa wanauawa katika mapigano hayo.

 


Tagi: vita , Yemen , Ethiopia

Habari Zinazohusiana