Shambulizi la bomu katika siku ya maulid Afghanistan

Shambulizi la kujitoa muhanga limepelekea vifo vya watu 43 katika mji mkuu wa Kabul nchini Afghanistan.

Shambulizi la bomu katika siku ya maulid Afghanistan

Shambulizi la kujitoa muhanga limepelekea vifo vya watu 43 katika mji mkuu wa Kabul nchini Afghanistan.

Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani Najib Danish amesema kuwa bomu hilo lilikuwa limelenga mkusanyiko wa watu wakisherehekea kuzaliwa kwa mtume Muhammad(SAW).

Takriban watu 43 wameauwa na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa.

Shambulizi hilo limeamsha hisia kubwa kwa wananchi nchini humo.

Mpaka sasa hakuna aliyetangaza kuhusika na shambulizi hilo.Habari Zinazohusiana