Rais Trump akataa kuzikiliza sauti ya mauaji ya Khashoggi

Rais wa Marekani Donald Trump akataa kusikiliza sauti iliorikodiwa wakati wa mauaji  ya mwanahabari Jmala Khashoggi

Rais Trump akataa kuzikiliza sauti ya mauaji ya Khashoggi

Rais wa Marekani Donald Trump akataa kusikiliza sauti iliorikodiwa wakati wa mauaji  ya mwanahabari Jmala Khashoggi.

Donald Trump , rais wa Marekani akataa kusikiliza sauti iliorikodiwa  wakati wa mauaji ya mwanahabari wa Saudia Jamal Khashoggi alipokuwa akiiuawa.

Trump amekiambia kituo cha habari cha Fox News kuwa hana haja kusikiliza sauti hizo zilizorikodiwa katika mahojiano aliofanya katika kituo hicho Jumapili.

Rais Trump amesema kuwa  sauti hizo ni za hudhuni na unyama hivyo basi hana haja kusikiliza sauti ambazo aanafahamu kilichotokea bila ya kuzisikiliza.

Jamal Khashoggi alionekana akiwa hai kwa mara ya mwisho alipokuwa akiingia katika ubalozi mdogo wa Saudia mjini Istanbul Oktoba 2.

 Habari Zinazohusiana