Uislamu barani Ulaya

Kutoka katika chuo kikuu cha Ankara Beyazıt kitengo cha Sayansi za Siasa Dr. Kudret BÜLBÜL

Uislamu barani Ulaya

Katika makala ya juma la mwisho, tulifanya tathmini ya Uislamu na tukasema kuwa tutaendelea wiki hii.

Kutoka katika chuo kikuu cha Ankara Beyazıt kitengo cha Sayansi za Siasa Dr. Kudret BÜLBÜL anatathmini mada yetu ya leo...

Katika muktadha wa Uislamu barani Ulaya, tumegusiaa baadhi ya waandishi wa Magharibi na kusema kwamba wanashughulikia suala hilo na kuchukua suala hilo kwa hali ya usalama. Na bodi za Halmashauri ya Kiislamu, zinajenga masuala ambayo yanaonekana kuwa ni shida.

Kwa kawaida, muundo wa bodi hii na wanachama wake vinaweza vikatofautiana na masuala yaliyotangulia hapo awali au mambo ambayo yamekuwa yakipitishwa mara nyingi na jambo hili huonekana kama tatizo kwa waislamu.Katika hali kama hii,waislamu wanatakiwa kujieleza kwa kina zaidi.

Bila shaka, kuna masuala mengi ambayo Waislamu wanaoishi Magharibi wanaweza kufanya ili kudhibiti mipango yao. Mimi nitasema tu kongamanao  la Kiislam ni muhimu.

Kongamano la kila mwaka

Kutokana na utaratibu wa utandawazi na malalamiko yanayosababishwa na malengo ya ubeberu kama vile ilivyo Syria, kuna uhamaji mkubwa wa wanadamu. Katika mchakato huu, maisha tofauti, ambayo kuna kipindi yalionekana kama hadithi za kale katika nchi za mbali, sasa yanaonekana kawaida.

Hali kama hii hii hujenga kiwango fulani cha kutokuwa na uhakika, wasiwasi, hofu. Katika mazingira kama hayo, kujieleza kwa wahamiaji kutaleta manufaa makubwa katika kuondoa yale wasiyoyataka na kupunguza wasiwasi katika maisha yao.


Katika hali hii, wasomi wa Kiislamu wanaoishi Ulaya wanaweza kufanya mikutano ya kila mwaka kwa kuunda jukwaa. Mikusanyiko hii inaweza kufanyika katika miji mikuu ya Ulaya, kama Paris, London, Berlin na Brussels.

Mikusanyiko inaweza kuwa juu ya masomo ambayo yatawasaidia waislamu kujieleza vizuri zaidi, pia wanaweza  kujadili maswala ya Ulaya au ya ubinadamu. Katika hali hii, ugaidi, ubaguzi wa rangi, kupambana na Uislam, uhuru wa kujieleza, elimu, familia, vijana, ushirikiano, matumizi ya madawa ya kulevya, mauaji ya wanafunzi  mashuleni,kuchukua watoto kwa lazima kutoka kwa familia zao ni kati masuala yanayoweza kuzungumziwa na kuzingatiwa.

Mbali na wasomi wa Kiislam, kushiriki kwa viongozi wakuu wa eneo husika ambapo mkutano utafanyika kama vile meya au gavana ,kushiriki kwa taasisi husika za mji huo na mamlaka ya serikali ni kati ya mambo ambayo yanaweza kuifanya mikutano hiyo kuwa na maana zaidi.

Kushiriki kwa mamlaka ya kiserikali katika mikutano kama hiyo kutasaidia kuonyesha kuwa mikutano hiyo sio ya kundi maalumu la watu na kwamba matatizo yanayozungumziwa katika mikutano hiyo ni matatizo ya wote na hivyo inakuwa ni rahisi kutafuta suluhisho.

Kutangaza kuwepo kwa mkutano kila mwaka ni jambo sahihi sana kwani kile kinachoonekana kuwa ni tatizo kitatafutiwa ufumbuzi.

Kwa nini wasomi wa Kiislam?

Bila shaka, mikusanyiko hiyo inaweza kuzingatiwa kati ya Waislamu  wawakilishi wa mashirika ya kiraia, biashara, utamaduni na wanasiasa. Inafaa kufanya mikutano kati yao. Hata hivyo, katika jamii, wasomi ni wale wanaoweza kukutana katika maeneo tofauti katika jamii husika, kuwasiliana na wananchi kiurahisi.

Kwa upande mwingine, masuala ya kujadiliwa katika mkutano yatakuwa na mitazamo mingi kama vile kidini, kijamii, kisaikolojia, taasisi za umma, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni.

Kutokana na hili, itakuwa vizuri zaidi kuwa na kongamano kama kikundi cha wataalamu na kuhusisha waalimu, wawakilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali, wafanyabiashara, utamaduni na wanasiasa.

Matunda ya kufanyika kwa mikutano kama hiyo

Mkutano huo ambao wasomi wa Kiislamu, viongozi wa serikali husika na vyama mbalimbali hushiriki mara nyingi huleta matokeo mazuri katika masuala mbalimbali.

Kwa jumuiya za Kiislamu: wasomi wa Kiislamu wanaoishi Ulaya, kwa bahati mbaya, huwa hawakutani katika jukwaa moja bali hujielezea kwenye majukwaa tofauti kama vile ya kikanda,kitaifa na ya kidini.

Ingawa matatizo ni jambo la kawaida barani Ulaya, ufumbuzi hutafutwa zaidi katika mila tofauti, uzoefu katika nchi na mashirika ya ndani.

Mkutano huo utawapa wasomi wa Kiislamu fursa ya kujadili matatizo yao kwa undani. Waislamu watazungumzia hali ya nchi, itikadi, kabila, madhehebu, dunia, jamii kama sehemu ya maisha mbalimbali.

Baadhi yao huwa na ufumbuzi, kutoka katika mila au nchi waliotokea (Marekani, Australia). Mkutano huo utakuwa na uwezo wa kuzaa matunda na kutoa suluhisho zenye maana.

Kwa upande mwingine,mikutano kama hiyo itaweka wazi majina ya viongozi ambao wanaweza kuzungumza kwa niaba ya waislamu.

Kongamano linatoa fursa ya kuamua kile wasomi wa Kiislamu wanaona kama tatizo kwao wenyewe na kile wanachopendekeza kama suluhisho.

Kwa upande wa mataifa husika, baadhi ya nchi nyingi zaidi za Waislam katika nchi zao ziko katika ajenda ya kuelewa, kujenga-suluhisho, na wengine kwa kusudi la kuhusisha na kuwaongoza Waislamu. Mkutano huo utasaidia mataifa yanayotaka kuzalisha ufumbuzi kwa imani nzuri kutatua matatizo ya kuishi pamoja.

Kutambua au kutatua tatizo kwa niaba ya Waislamu kunasaidia kutengeneza ufumbuzi ambao hautachukiwa, au tuseme kulazimishwa.

Suala likitatuliwa na watu wengine basi linaweza kuleta wasiwasi katika jamii ya kiislamu kinyume na inavyokuwa pale tatizo linapochambuliwa na muislamu mwenzao.

Ikiwa wasiwasi wa Kiislam haujajibiwa moja kwa moja na wasomi wa Kiislam,basi  utajibiwa na wengine kwa njia mbaya na ambayo mara nyingi si sawa.

Katika muktadha huu, mikutano kama hii inaweza kufanyika katika maeneo kama Afrika, Balkans, Australia nk. Nchini Marekani, ingawa siyo hasa kwa maana hii, kuna baadhi ya mikutano yenye mcahngo sawa na huu.


Kutoka katika chuo kikuu cha Ankara Yıldırım Beyazıt kitengo cha Sayansi za Siasa Dr. Kudret BÜLBÜL ametufanyia tathmini ya mada yetu ya leo.


Tagi: Ulaya , uislamu

Habari Zinazohusiana