Moto mkubwa waleta maafa jimboni California

Moto mkubwa wazuka jimboni California nchini Marekani

Moto mkubwa waleta maafa jimboni California

Moto uliozuka msituni katika jimbo la California nchini Marekani umesababisha vifo vya watu 5.

katika taarifa iliyotolewana ofisi ya mkuu wa polisi wa eneo la Butte inasema kilomita 290 kaskazini mashariki mwa San Francisco, kijiji cha Paradise walikuta miili mitano ya watu waliofariki, ikiwa ndani ya magari yaliyoungua.

Mkurugenzi wa Huduma ya kwanza wa jimbo la California Mark Ghilarducci amesema kutokana na moto huo wamewataka kuhama makazi yao watu zaidi ya laki moja na nusu, vilevile wamezitaka mamlaka husika kuimaimarishwa timu za uokoaji katika maeneo ya karibu kama Oregon, Nevada na Arizona.

Kapteni Scott McLean kutoka komandi ya zima moto ya California akizungumza siku ya Alhamisi alisema, Kutokana na moto huo kijiji cha Paradise chenye idadi ya watu wapatao 27,000 majenfo zaidi ya elfu moja yameharibiwa vibaya kabisa, na watu zaidi ya elfu 10 wamelazimika kuyahama makazi yao.

 

 


Tagi: Moto , Marekani

Habari Zinazohusiana