Mafuriko nchini Jordan

Watu 11 wamepoteza maisha katika mafuriko yaliosababishwa na mvua kubwa nchini Jordan.

Mafuriko nchini Jordan

Watu 11 wamepoteza maisha katika mafuriko yaliosababishwa na mvua kubwa nchini Jordan.

Msemaji wa Serikali ya Jordan Cumane Guneymat, katika taarifa yake iliyoandikwa, amesema kuwa mafuriko hayo yaliyosababishwa na kunyesha kwa mvua kubwa yamepelekea watu 11 kupoteza maisha na wengine wawili kupotea.

Shughuli ya utafutaji  na uokoaji inaendelea.

Shirika la habari la Jordan, PETRA, limetangaza kuwa vitengo vya jeshi vimepewa kazi ya kutafuta  na kuokoa watu baada ya mafuriko hayo.

Mvua kubwa nchini humo ilipelekea watu 21 kupoteza maisha mwezi uliopita.


 Habari Zinazohusiana