Msafara wa waziri mkuu wa Uingereza wapata ajali

Msafara wa waziri mkuu wa Uingereza bi Theresa May wapata ajali nchini Ubelgiji

Msafara wa waziri mkuu wa Uingereza wapata ajali

 

Msafara wa waziri mkuu wa Uingereza bi  Theresa May umepata ajali ya barabarani nchini Ubelgiji.

Waziri huyo mkuu wa uingereza yupo nchini Ubelgiji kwenye mkutano wa umoja wa Ulaya unaojadili kujitoa kwa Uingereza kwenye umoja huo mchakato uliobatizwa jina Brexit.

 

Katika taarifa iliyoripotiwa na gazeti la Ubelgiji "La Libre Belgique" inasema hakuna aliyepoteza maisha kwenye ajali hiyo, polisi wawili walijeruhiwa kutokana na ajali hiyo.

Waziri mkuu wa Ubelgiji, Michel, naye pia alikuwepo kwenye msafara huo, limeripoti gazeti hilo.

 Habari Zinazohusiana