Waziri wa ulinzi wa Uturuki na uamuzi wa Marekani dhidi ya kundi la PKK

Waziri wa ulinzi wa Uturuki Hulusi Akar asema kwamba Marekani inasubiriwa kuchukuwa hatua dhidi ya kundi la YPG kama ilivyofanya dhidi ya PKK

Waziri wa ulinzi wa Uturuki na uamuzi wa Marekani dhidi ya kundi la PKK

Hulusi Akara, waziri wa ulinzi wa Uturuki amezungumza kuhusu uamuzi uliochukuliwa na Marekani kuhusu kundi la wangambo wa PKK.

Kufuatia uamuzi huo, Hulusi Akar amesema kwamba Uturuki inasubi kuona Marekani inachukuwa uamuzi dhidi ya kundi la wanagambo wa YPG kama ilivyochukuwa dhidi ya kundi la wanmagambo wa PKK.

Uturuki inalitambua kundi la YPG kama tawi la kundi la wanamgambo wa PKK.

Hulusi Akar ameyazungumza hayo akiwa katika kisiwa cha Suakin nchini Sudani katika ziara yake .

Ifahamike kuwa Marekani imetangaza donge nono la pesa kwa mtu yeyote atakaetoa taarifa zitakazopelekea kukamatwa viongozi watatu wa kundi la PKK.

Kwa mujibu wa Uturuki uamuzi huo wa Marekani ni uamuzi wa pongezwa licha ya kuchelewa kwake.Habari Zinazohusiana