Watu 12 wauawa katika makabiliano ya silaha California Marekani

Watu 12 wafariki katika makabiliano ya silaha  katika ukumbi wa starehe  California nchini Marekani

Watu 12 wauawa katika makabiliano ya silaha California Marekani

Watu 12 akiwemo mshambuliaji wafariki katika makabilaiano ya silaha yaliotokea katika ukumbi wa starehe Thousand Oaks California nchini Marekani.

Mtu mmoja aliekuwa silaha aliingia katika ukumbi wa starehe Thousand Oaks na kuanza kufyatua risasi  hovyo katika umati wa watu waliokuwa katika  ukumbi huo.

Vyanzo vya habari kutoka katika eneo la tukio  vimefahamisha kwamba watu zaidi ya 15 wamejeruhiwa katika  tukio hilo.

Hakuna taarifa zaidi ambazo zimetolewa  kuhusu tukio zaidi ya kufahamishwa kuwa mtu aliendesha shambulizi hilo aliuawa  katika makabiliano na  polisi walinda usalama.Habari Zinazohusiana