Waziri Çavuşoğlu kufanya ziara Laos

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki  Mevlüt Çavuşoğlu anatarajia kufanya ziara.

Waziri Çavuşoğlu kufanya ziara Laos

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki  Mevlüt Çavuşoğlu anatarajia kufanya ziara.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na wizara hiyo,Çavuşoğlu atatembelea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Laos tarehe 7-8 Novemba.

Katika ziara  yake kwa mara ya kwanza Laos,waziri huyo atakutana na waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Saleumxay Kommasith na kufanya nae majadiliano mbalimbali ikiwemo mada ya kudumisha uhusiano na ushirikiano baina ya mataifa hayo mawili.

Viongozi hao pia watabadilishana mawazo kuhusu masuala tofauti ya kimataifa.

Waziri Çavuşoğlu atapokelewa na waziri mkuu wa Laos Thongloun Sisoulith.Habari Zinazohusiana