Tume ya umoja wa Ulaya yaridhia Disney kuinunua 21st Century Fox

Tume ya umoja wa Ulaya yaridhia Disney kuinunua 21st Century Fox, baada ya disney kutii masharti yaliyowekwa na umoja huo

Tume ya umoja wa Ulaya yaridhia Disney kuinunua 21st Century Fox

Tume ya umoja wa Ulaya imeridhia ombi la shirika kubwa la habari na buradani,Disney,kununua shirika la " 21st Century Fox" kwa thamani ya dola za kimarekani milioni 71,3.

Katika taarifa iliyotolewa na tume hio wamekubali baada ya Disney kutii masharti yote yaliyowekwa na tume hio. Masharti yaliyowekwa na umoja wa Ulaya yalikuwa ; Ili disney iweze kulinunua shirika la 21st century Fox, Disney ilihitajika kuuza mashirika ya televisheni inayoyaendesha barani Ulaya kama vile History, H2, Crime & Investigation, Blaze na Lifetime.

Maridhiano haya ya manunuzi ya dola milioni 71,3 yataipa Disney haki ya kumiliki studio za filamu za 21st Century Fox, pamoja na haki za usambazaji wa X-Men, Avatar, Simpsons na National Geographic.

 

 Habari Zinazohusiana