Macron atoa wito wa kuundwa jeshi la Ulaya bila ya kushiriki Marekani

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron atoa wito wa kuundwa jeshi la Ulaya bila ya kushirikisha Marekani

Macron atoa wito wa kuundwa jeshi la Ulaya bila ya kushiriki Marekani

Emmanuel Macron, rais wa Ufaransa ametoa wito wa kunndwa kwa jeshi la Ulaya bila  ya kushirikisha Marekani. Kwa mujibu wa rais wa Ufaransa, jeshi ni kwa ajili ya kukabiliana na vitisho kutoka nchini Urusi.

Pendekezo hilo kutoka kwa rais wa Ufaransa limetolewa Jumanne akifahamisha kuwa ni kwa lengo la kuimarisha usalama barani Ulaya kutokana na vitisho vya Urusi.

Hayo rais wa Ufaransa aliyazungumza  katika mahojiano aliofanya katika kituo cha  redio cha « Europe 1 »

Rais Macron amesema kuwa umesema kuwa kuna umuhimu mkubwa kwa Ulaya kujilindia usalama .

Macron ametahadharisha  kuenea kwa  sera za kizalenda ambazo zinatoa ujumbe wa kutisha barani Ulaya.

Rais wa Ufaransa amemalizia akisema kuwa  matamshi ya rais wa Marekani Donald Trump na uamuzi wake ni tishio kwa usalama wa Ulaya.Habari Zinazohusiana