Chanzo cha Marekani kurejesha vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Iran

Chanzo cha Marekani kurudisha vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Iran na athari ya vikwazo hivyo

Chanzo cha Marekani kurejesha vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Iran

 

Marekani iliamua kuvirejesha vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Iran. Mwanzoni mwa wiki hii vikwazo hivyo vimeanza kutumika tena. Vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Iran viliondolewa baada ya mktaba wa Nyuklia wa mwaka 2015 kusainiwa katika medani ya kimataifa.

Mkataba ule uliitaka Iran iweke mipaka kwenye shughuli zake za kinyuklia.Iran ilitii mkataba ule hivyo jumuiya ya kimataifa ilisaini mkataba ule na kuiondolea Iran vikwazo. Utawala wa rais Trump ili kuweza kuvirudisha tena vikwazo hivi mnamo mwezi Agost ulitangaza awamu ya kwanza ya vikwazo na hivi sasa umetangaza awamu ya pili ya vikwazo hivyo.

Uamuzi huo unaukandamiza  uchumi wa Iran. Unaiwekea mipaka katika biashara ya nje na ndani. Kwa upande mwingine zipo nchi ambazo zilikuwa zikifanya biashara, hasa katika sekta ya nishati, na nchi ya Iran.

Je maamuzi haya ya kuiwekea vikwazo Iran yataziathiri vipi nchi hizi ? Uturuki nayo kama moja wa nchi nane ambazo hazijajumuishwa kwenye vikwazo (Itaruhusiwa kuendelea na biashara na Irani)  inalichukuliaje suala  hili ?

Mkufunzi  Idara ya uchumi, kitivo cha elimu ya siasa  chuo kikuu cha Yıldırım Beyazıt Prof. Dr. Erdal Tanas KARAGÖL anatufafanulia...

Chanzo cha kurudisha tena vikwazo hivi dhidi ya Iran ni Utawala wa Trump kufikiri kwamba Iran imeacha kuzuia shughuli za kinyuklia za kikanda. Ifahamike wazi kwamba mataifa mengine ambayo yalikuwamo kwenye makubalino yale kama China, Urusi, Ufaransa, Uingereza, Ujerumani, yanaonyesha yameegemea upande wa kuendelea na makubaliano yale.

Inabidi kusema pamoja na kuonyesha msimamo huo, mshirika ya kimataifa hayajaonyesha msimamo wa aina hiyo. Baada ya kutangazwa uamuzi wa vikwazo mashabiki wa mkataba ule walianza kujiondoa katika soko la Iran mmoja baada ya mwingine.

Hili pia linaonyesha, katika medani ya kimataifa mtizamo kuhusiana na Iran kwa upande wa kidiplomasia na kwa upande wa sekta binafsi  vinatofautina sana.

Katika hatua ya mwanzo ya vikwazo vilivyoanza mnamo Agosti 7 mpaka hivi sasa, serikali ya Iran ilizuiwa kununua dola za kimarekani, ilizuiwa kufanya biashara kwa kutumia dhahabu vilevile viliwekwa vikwanzo katika kufanya biashara kwa kutumia sarafu ya kitaifa. Soko la nje la Iran lilianza kuparaganyika kwa nchi moja moja kuanza kusimamisha kufanya biashara na Iran.

Sasa awamu ya pili ya vikwazo vya kibiashara dhidi ya Iran imeanza kutumika. Inaweza kusemwa awamu hii inagusa sekta mtambuka ya uchumi wa Iran, yaani biashara ya nishati kwa upande mwingine inagusa sekta ya uchumi na usafirishaji kwa njia ya meli.

Nchi ambayo ina hifadhi kubwa ya mafuta na gesi asilia duniani kama Iran, Inapowekewa vikwazo vya kibiashara vinavyolenga sekta hii ya nishati inamaanisha muelekeo wa  sera za nishati katika ukanda huu zitaathirika kwa kiwango kikubwa. Hılo litafuatiwa na athari kuonekana katika soko la nishati la ulimwengu.

Sehemu kubwa ya watu wa Iran kipato chao kinategemea mapato yatokanayo na biashara ya mafuta. Kwa maneno mengine tunaweza kusema waziwazi kwamba uchumi wa Iran unategemea mapato yatokanayo na bishara ya mafuta. Kwa mtazamo huo kuweka vikwazo katika sekta hii mtambuka kutazuia kwa kiasi kikubwa mkondo wa mitaji na kuyumbisha kwa kiwango kikubwa  uchumi wa taifa hili.

Je nyuma ya maamuzi haya ya Marekani ya vikwazo dhidi ya Iran, msukumo mkuu ni nini ?  Kwanza kabisa Iran ikiwa kama nchi yenye hifadhi kubwa ya mafuta na gesi asilia, Ina nafasi kubwa sana ya kuwa na nguvu ya kiuchumi na kisiasa ikiweza kufikisha nishati hii maeneo inapohitajika. Sasa ukijumlisha nguvu hii ya kiuchumi inayoweza kuipata Irani na uwezo wa kinyuklia inakuwa ni tishio kubwa kwa Marekani na washirika wake.

Kwa upande mwingine ukizingatia kwamba Iran inatawala mlango bahari wa Hormuz, ambao unatajwa kupitisha asilimia 30 ya mafuta yote duniani ,yote hii inaweza kuelezea tabia inayoonyeshwa kwenye medani ya kimataifa dhidi ya Iran.

Mwisho kabisa siku ya Jumatatu ilitolewa orodha ya nchi ambazo zitaruhusiwa kufanya biashara na Iran ( hazipo kwenye vikwazo) na moja wapo ni Uturuki. Maamuzi hayo tunaweza kuyaelezea kama muhimu sana kwa Uturuki kwa vile yanailinda biashara yenye thamani ya dola za kimareki bilioni 10.6 lakini kwa upande mwingine pia yatalinda uelekeo wa sera ya nishati ya Uturuki lakini pia usalama wa upatikanaji wa nishati katika ukanda huu.

Mkufunzi  Idara ya uchumi, kitivo cha elimu ya siasa  chuo kikuu cha Yıldırım Beyazıt Prof. Dr. Erdal Tanas KARAGÖL anatufafanulia.Habari Zinazohusiana