Marekani kujiondoa katika makubaliano ya nyuklia na Urusi

Rais Trump asema Marekani itajitoa kwenye makubaliano yake na Urusi kuhusu silaha za nyuklia

Marekani kujiondoa katika makubaliano ya nyuklia na Urusi

Rais wa Marekani Donald Trump amesema ataiondoa nchi yake kwenye makubaliano waliokubaliana na Urusi kuhusu silaha za nyuklia.

Rais Trump aliyasema hayo jumamosi alipopngea na wanahabari baada ya kampeni katika jimbo la Nevada.

Makubaliano hayo yajulikanayo kama makubaliano ya silaha za kinyuklia za masafa ya kati "Intermediate Range Nuclear Forces (INF)" ambayo yalifanywa mwaka 1987 kati ya Marekani na  muungano wa kisovieti,USSR ya wakati huo.

Makubaliano haya yaliondoa silaha zote za nyuklia na mitambo ya kurushia makombora ya nyklia yenye uwezo wa kurusha umbali wa mail 310  hadi mail 3,420 (km 500 hadi km 5,500)

Rais Trump alisema Urusi wamevunja makubaliano hayo, hivyo Marekani itajitoa kwenye makubaliano hayo.

Trump alimkosoa mtangulizi wake rais Obama kuwa aliendelea na makubaliano hayo ili hali Urusi wao wameyavunja kwa kutengeneza silaha ambazo zimekatazwa na makubaliano hayo. Makubaliano hayo yanafanya iwe vigumu kwa Marekani kutengeneza silaha hizo zilizozuiwa.

Rais Trump hajasema lini Marekani itajitoa kabisa katika makubaliano hayo.Habari Zinazohusiana