Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki alinganisha kiwango cha misaada kutoka Uturuki na Marekani

Ututuki inatumia karibu kiasi sawa na inachotumia Marekani katika misaada ya nje

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki alinganisha kiwango cha misaada kutoka Uturuki na Marekani

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Çavusoğlu, akiongea katika ufunguzi wa mwaka wa masomo wa chuo kikuu cha New York Tirana, mnamo siku ya alhamisi mji mkuu wa Albania, Tirana, alisema kwamba katika misaada ya kibinadamu Uturuki inatoa karibu kiasi sawa na kiasi inachotoa nchi ya Marekani ambayo ndio nchi yenye mapato makubwa zaidi duniani.

Alitolea mfano mnamo mwaka 2017 Uturuki ilitoa kiasi cha dola za kimarekani bilioni 8 kusaidia wakati Marekani yenyewe ilitoa kati ya dola bilion 6 na 7.Alisema Uturuki ni nchi ambayo ipo katika daraja la juu kabisa katika masuala ya misaada ya kibinadamu.

 Aliendelea kutoa mifano akisema mwaka 2016 Marekani ilitumia kiasi cha dola bilioni 6.3 katika misaada  wakati Uturuki ikitumia dola bilioni 6 na kuifanya Uturuki ishike nafasi ya pili katika kutoa misaada baada ya Marekani.

 Habari Zinazohusiana