Kanuni za kimataifa za elimu

Ni upi mkatati wa Elimu? Kutoka katika chuo kikuu cha Ankara Yıldırım Beyazit, kitengo cha siasa, Daktari  Kudet BÜLBÜL

Kanuni za kimataifa za elimu

Wakati  waziri wa elimu m Ziya Selçuk alipoanza  mpango wake, kulinekana kuwa kulikuwa na umuhimu wa mfumo wa kimkakati ambalo likuwa ukihtajika katika kipindi  cha muda mfupi na kuanza kwa  kubadilishana fikra kama ilivyokuwa matarajio ya watu wengi.

Tunafahamu kuwa miongoni mwa changamoto zinazotukabili  katika vyuo  ni uongozi na mfumo  ambao umeambatana na ukosefu wa  mikakati. 

Kutokana na sababu hizo kuna umuhimu mkubwa kuanza na utafiti ambao utapelekea kufikia katika mikakati katika mfumo wa uongozi katika  taasisi za serikali na  binafsi.

 Katika kipindi kifunpi kulikuwa na muonekano katika  mfumo wa elimu uliokuwa  ukihştaji mabadiliko  ya kiufundi na matatizo yaliokuwa yakitokea katika kpindi cha dharura.

Bila shaka kunahitajika  mkakati mpya.  Kwa upande mmoja au mwingine, miongoni mwa matatizo yanaytukabili katika mfumo wa elimu ni mikakati mibuvu isiokuwa na muelekeo.  

Licha ya kuwa utafiti  wa kufikia  katka mikakati  imekwishakuwa tayari tunatakiwa   kutoa mchango  kwa pamoja ili  isijekuwa  mikakati  mibovu katika kipindi cha miaka 200.

Kutoka katika chuo kikuu cha Ankara Yıldırım Beyazit, kitengo cha siasa, Daktari  Kudet BÜLBÜL anatafafanulia…

        1. mkakati ambao  unakwenda sambamba na  maslahi na mahitaji ya binadamu:  Mkakati wa mafunzo  unatkiwa kuwa  na muelekeo ambalo malengo yake ni kuwa  na  maslahi katika jamii na binadamu ili kupelekea jamii yetu  kuwa  na taifa ambalo  lina matumaini na wakati ujao.  Maslahi  ya binadamu

Mkatati wa  elimu na mafunzo  unatakiwa kuwa na usawa na mahitaji katika jamii  na kuwa pia na maslahi katika jamii inayolengwa.

Hali hiyo ni kwa ajili ya kulifkisha taifa katika atua ambayo ilkuwa ikitarajiwa kwa muda mrefu.  Maslahi ya ubşnadau yanatakiwa kupewa  umuhimu chini ya misingi ya kiimani, kitamaduni na  mwenendo ambao unalijenga taifa.

       2. Mkakati  na kanuni za msingi : Baada ya maslahi   ya binadamu  katika mafunzo  na kufuata mafunzo ya wanafalsafa na kanuni za msingi ,  katika  makala zilizopita tulijadili kuhusu mfumo wa elimu , tulainagalia pia kanuni 7: elimu ambayo inashawishi  muamko na kutetea haki na usawa,  elimu anayofanya binadamu kuwa huru na kuwa na mtazamo chanya katika kila ambo.   Kuna utofauti   kwa watu  ambao  elimu pia ni tofauti kutokana na  ujuzi na pia kutokana na fursa.

      3. Uchambuzi  wa mahitaji  yanayostahili :  baara ya  uinaddamu kupewa kipaumbele  tunatakiwa kuchambua  usahihi na usawa ambao unakenda sambamba na  masharti na kanuni  zilizoendana na wakati uliopo. 

Mahitaji yalopo ni mahitaj ambayo  ynatakuwa kuwa sambaba na wakati ujao wa Uturuki kutokan ana malengo ilioiwekea katika sekta tofauti ili ufika katika maendeleo.

Sio tu kwa Uturuki bali katika maeneo tofauti ulimwenguni katika sekta  binafsi , katika uzio wa wasomi,  mashirika  na taasisi zisizokuwa za kiserikali, mashirika tofauti pia  katika muendelezo .  kunatakiwa pia kutoa kipaumbele katika  mafunzo ambayo yanafundisha taaluma  na kufanyia maerkebesho kutokana na mahitaji katika jamii husika.

      4.Mkakatı usio tawala bali unaoratibu na kuingoza jamii: Pindi tu ule muelekeo unaohitajika, kanuni pamoja na njia zikiwa zimeshafahamika. Suala la muhimu linakuwa ni je mafunzo haya yote yatafanywa na jamii au jamii yenyewe itachukua nafasi yausimamizi tu na uratibu.

Katika dunia ya sasa watu wanataka waweze kuamua kuhusu hatima ya watoto wao; kipindi cha vita baridi ambapo taifa lilikuja na mtaala ambao ilipanga bila kujali matakwa ya wananchi kimepitwa na wakati. Familia zinaangalia aina ya elimu inayowafaa watoto wao kulingana na dini, lugha na utamaduni.

Ukizingatia mchakato wa utandawazi uliopo muelekeo unaohitajika katika soko ni zaidi ya elimu sare iliyotolewa wakati wa vita baridi. Mfumo wa elimu inabidi uweze kujibu matakwa haya tofauti ya familia pamoja na matakwa tofauti ya soko .

Kwa hio kuandaa mkakati wa mafunzo pia ni suala la uhuru, haki za binadamu na matakwa ya soko.

Zaidi mfumo wa elimu inabidi uweze kujibu matakwa ya familia kama wanataka iwe elimu ya kiislamu zaidi,kikiristo zaidi, kiyahudi zaidi, kipagani zaidi, huru zaidi, ya kijamaa zaidi, isiyobadilika zaidi na mahitaji mengine ya kielimu. Wakati huo huo katika mazingira ya kidunia ambapo ushindani unaongezeka mahitaji inabidi yaendane na mabadiliko ya mara kwa mara ya soko. Sio rahisi kwa elimu kwa umma iliyopo kuweza kujibu mahitaji hayo tofauti ya familia na mabadiliko ya mara kwa mara ya soko.

Hivyo basi Mkakati wetu wa elimu usiwe wa kutekelezwa na umma bali unaoratibiwa , kusimamiwa na kuongozwa na umma. Hali iliyopo yakuongeza ushirikishwaji wa sekta binafsi na jamii katika elimu izidishwe.

( Katika sekta ya afya njia hii inaweza kutumika pia kwa mafanikio).Unaweza kutaja makosa ya asasi za kiraia na sekta binafsi.

Ukosoaji huu unaweza kuwa sawa. Lakini utamaduni wetu ni katika mama ya tamaduni. Wakina Ibn Sina, Gaza, Mevlana, Harezmi, Mola Fenari, yote ni majina yanafanya sehemu ya utamaduni wetu mama ya tamduni , hata kama mto ulikuwa unaelekea kukauka inatubidi tubebe kupeleka kwa mto huu ili uendelee kutiririka.

Kwaupande mwingine kwa  nchi kama Uturuki ambazo zina idadi kubwa ya vijana lakini kasi ya kuongezeka kwa idadi ya watu imepungua suala la kwamba serikali peke yake ndio iwezekeze kwenye elimu mfano kujenga shule mpya, kuongeza walimu wapya sio sawa kiuchumi.

Kutokana na kwamba idadi ya kuzaliana imepungua inamaanisha baada ya muda mfupi shule mpya na madarasa mapya hayatahitajika na kwamba walimu hawatapata wanafunzi wa kuwafundisha. Kwa hio suala la kuchandia hizi gharama na sekta binafsi ni la uhitaji kwa sababu za kiakili.

         5. Mkakati ambao unawaongoza wanafunzi kulingana na vipaji na karama zao kuliko ule unaotaka tu wafike mwisho: Moja ya matatizo makubwa ya mfumo uliopo wa elimu ni kwamba hauongozi wanafunzi kulingana na vipaji bali unabe tu wanafunzi kutoka shule za awali mpaka milango ya vyuo vikuu kasha baada ya hapo mitihani ya fani maalum.

Ukizingatia kwamba uhitaji wa nchi kwa utaalamu wa fani kazaa ni wa kiasi kidogo kwa hio ni hasara kwa nchi na kwa vijana pale watapomaliza vyuo na kukuta kwamba kazi hazipatikani.

Kwa sababu hiyo basi mkakati wetu wa mafunzo inabidi uwe unaongoza watoto kutoka shule za awali kulingana na uwezo na vipaji vyao.Mfumo huu wa kuongoza pia inabidi ujumuishe kuwa na uwezo wa kubadili kutoka muda hadi muda.

         6. Mkakati unaozingatia ushindani wa kimataifa;  Uturuki inakuwa kituo muhimu kwa wanafunzi wa kimataifa kadri siku zinavyokwenda. Wakati wa ufunguzi wa taasisi ya elimu ya juu YÖK rais wetu alisema kwamba Uturuki kuna wanafunzi wa kimataifa 143,000.

Ili kushindana kidunia namba hii tunataka tuiongeze. Ili kuweza kuvutia wanafunzi wengi zaidi wa kimataifa mkakati wetu wa elimu inabidi ufanye wanaofanya kazi katika sekta ya umma wawe na ufahamu mkubwa.

Kuwa na vyuo vikuu vya kibingwa, na sekta ya binafsi iwekeze zaidi, pamoja na kuingalia upya mitaalaya kufundishia. ( Wanafunzi wengi wa kimataifa wanaanguka katika somo la histori ya Uturuki sasa inabidi kutazama upya kuna haja wanafunzi wa kimataifa wachukue kama la lazima historia ya uturuki au wafundishwe somo hili kama wanavyofundishwa wanafunzi wazawa)

         7. Mkakati uwe unazingatia matakwa maeneo anayotoka: Mkakati uangalie mahitaji ya kitongoji husika,vitongoji tofauti vitoe fursa za shule za aina tofauti. Shule ziwe zinafunguliwa katika vitongoji kulingana na mahitaji ya vitongoji hivyo.

Nimalize kwa kutumia maneno ya Mkurugenzi mkuu wa Alibaba Jack Ma “Elimu ni tatizo kubwa, kama hatutabadilisha jinsi tunavyo fundisha tunaweza kuwa kwenye matatizo makubwa kwa sababu jinsi tunavyofundisha kumepitwa na wakti kwa miaka 200.

Hatuwezi kuwafundisha watoto wetu washindane na mashine, Wao wana akili zaidi. Maadili, Imani, Fikra huru, kufanya kazi kwa kushirikiana na kuheshimu watu wengine hivi ni vipawa vya binadamu.Elimu haiukufundishi vitu hivi.

Ili watu waweze kuelewa kwamba wao wanatofautina inabidi tuwafundishe sanaa. Tunachofundisha inabidi kiwe tofauti na mashine”.

Mkuu wa kitivo cha elimu ya siasa chuockikuu cha Yıldırım Beyazit Ankara Prof. Dr. Kudret BÜLBÜL kuhusiana na mada hii anatuchambulia..

 Habari Zinazohusiana