Ziara ya rais Erdoğan nchini Moldova

Rais wa Uturuki ajielekeza nchini Moldova kat,ka ziara yake ya siku  mbili

Ziara ya rais Erdoğan nchini Moldova

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan ajielekeza nchini Moldova ambapo anatarajiwa kufanya ziara mabyo itachukuwa muda wa siku mbili.

Katika ziara yake hiyo nchini Moldova, rais Erdoğan atakutana na kufanya mazungumzo na waziri mkuu wa nchi hiyo  Pavel Filip.

 Vile vile rais Erdoğan atakutana na  mawaziri  wa nchi hiyo ili kuzungumza kuhusu ushirikiano kati ya Uturuki na Moldova katika sekta tofauti. Ziara hiyo imeanza rasmi Oktoba 17 na inatarjiwa kumalizika  Oktoba 18.

Taar,fa kuhusu ziara hiyo ya rais Erdoğan ametolewa na  chanzo cha habari kuto0ka ikulu mjini Ankara Jumanne.

Rais Erdoğan anajielekeza nchini Moldova baada ya kualikwa na rais  Igor Dodon.

Katika jimbo la Gagauzia, rais Erdoğan atakutana na gavana wa jimbo hilo Irina Vlah na kufanya mazungumzo. Katika mikutano ambayo rais wa Uturuki atafanya na viongozi tofauti wa Moldova, suala zima lla ushirikiano  katika sekta ya biashara litazungumziwa.

Kiwango cha ushirikiano klatika sekta hiyo kinakadiriwa kuwa dola bilioni 1,5.

Mapambano dhidi ya  ugaidi na kundi la wahaini wa FETÖ ni moja ya masuala yatakayo zungumziwa pia kati ya rais Erdoğan na viongozi wa usalama Moldova.

Rais Erdoğan atakutana na viongozi wa mashirika tofauti ya kituıruki  213 ambayo yamewekeza kiwango cha dola  milioni 350 nchini humo.

 Habari Zinazohusiana