Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya - hakuna maridhiano

Kikao cha mabalozi wa Umoja wa ulaya cha kujadili kujitoa Uingereza kwenye Umoja huo chamaliza bila maridhiano

Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya - hakuna maridhiano

Mabalozi 27 wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya walikutana mjini Brusels Ubelgiji kwenye kilele cha kujadili kujitoa  Uingereza(Brexit) kwenye Umoja huo.

Katika mkutano matokeo ni kwamba maridhiano hayakufikiwa.

Uingereza na Umoja wa Ulaya wameshindwa kufikia muafaka kwenye majadiliano.

Tume  ya Umoja wa Ulaya ilitoa taarifa kwamba  iliitisha kikao cha mabalozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya lakini ubalozi wa Uingereza, haikujumuishwa kwenye kikao hicho.

Matokeo ya majadiliano hayo ni kwamba hakuna maridhiano, kikao hicho kitaendelea siku ya jumatano.

Katika ukurasa wake wa Twitter balozi wa Ufaransa ambaye ndiye kiongozi wa majadiliano hayo alisema  kuwa pamoja na juhudi zote lakini bado yapo mambo ambayo hatujakubaliana moja wapo likiwa suala la mpaka wa Kaskazinİ wa Ireland.

Mbunge wa Uingereza pamoja na Jamhuri ya Kidemokraria ya Ireland Kaskazain Nigel Dodds amesema kiburi cha Umoja wa Ulaya ndio kitakachofanya Uingereza ijitoe kwenye Umoja huo bila kufikia maridhiano na kuligeuza suala la Ireland Kaskazini kuwa vita ya Umoja huo.

Uingereza inatarajiwa kujitoa rasmi kwenye Umoja huo ifikapo Mei  mwaka 2019.

 

 Habari Zinazohusiana