Rais wa Marekani apongeza ushirikiano wa rais Erdoğan kuhusu Brunson

Rais Donald Trump apongeza ushirikiano wa rais Erdoğan kufuatia suala zima la kuachwa huru kwa Andrew Brunson

Rais wa Marekani apongeza ushirikiano wa rais Erdoğan kuhusu Brunson

Rais wa Marekani Donald Trump amekana  kuwa kuachwa huru kwa mchungaji Brunson na kurejea nchini Marekani kumeafikiwa baada ya makubaliano kati ya Uturuki na Marekani.

Rais Trump ametoa shukrani kwa msaada  kutoka kwa rais Erdoğan.

Trump aliandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa  atakutana na Brunson  Jumamosi  White House.

Kufuatiwa kuachwa huru kwa Brunson, Trump amesema kuwa ushirikiano kati ya Uturuki na Marekani utaendelea kama ilivyokuwa hapo awali. 

Mahakama mkaoni Izmir nchini Utururuki Ijumaa alimuacha huru Andrew Brunson ambae alikuwa amehukumiwa adhabu ya kifungo  baada ya kukutwa na hati ya kushirikiana na makundi ya kigaidi.Habari Zinazohusiana