Rais wa Marekani kutoa shukrani kwa rais Erdoğan

Rais wa Marekani Donald Trump kutoka shukrani kwa rais wa Uturuki baada ya mchungaji Brunson kuachwa huru

Rais wa Marekani kutoa shukrani kwa rais  Erdoğan

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan ajibu ujumbe wa rais wa Marekani Donald Trump  aliondika katika ukurasa wake wa Twitter.

Rais wa Uturuki amefahamisha kuwa sheria imefuata mkondo wake bila ya  shinikizo la aina yeyote kuhusu sakata za mchungaji Andrew Brunson kuachwa huru.

Rais Erdoğan amejibu ujumbe wa rais wa Marekani katka ukurasa wake wa Twitter. Katika ujumbe wa rais Erdoğan akimjibu rais Trump amesema kuwa mahakama ya Uturuki imechukuwa uamuzi wake chini ya misingi ya sheria bila ya shinikizo laiana yeyote na kuendelea kusema kuwa  anayo matumaini kuwa  ushirikiano kati ya Uturuki na Marekani utandelea.

Katika ujumbe huo amefahamisha mapambano dhidi ya makundi ya ugaidi kama PKK, Daesh na FETÖ yataendelea kwa ushirikiano na Marekani.

Kwa uapnde wake rais Trump amesema kuwa itakuwa ni furaha kumpokea Brunson na kutoa shukrani kwa rais Erdoğan.

 Habari Zinazohusiana