Mgogoro wa kidiplomasia kati ya Urusi na Uingereza waibuka upya

Mgogoro kati ya Urusi na Uingereza waibuka upya baada ya Urusi kuamua kujibu mapigo

Mgogoro  wa kidiplomasia kati ya Urusi na Uingereza waibuka upya

Baada ya Uingereza kutangaza kwamba haitawapa viza wanadiplomasia wa Urusi, Urusi nao wamejibu mapigo kwa kusema nao hawatawapa viza wanadiplomasia wa Uingereza.

Hilo limefungua sura mpya ya mgogoro wa kidemokrasia kati ya Urusi na Uingereza.

Balozi wa Urusi anaehudumu nchini Uingereza Aleksander Yakovenko alisema kwamba kutokana na ule mgogoro  uliobuka baina ya nchi hizi mbili kuhusiana na kulishwa sumu akina Skripal. Wanadiplomasia waliofukuzwa kutoka Uingereza wananyimwa viza kurudi tena nchini Uingereza "Kutokana na serikali ya Uingereza kutotoa viza kwa wanadiplomasia wetu, tunashindwa kuzijaza nafasi hizi" alisema.

Kuhusiana na suala hili Urusi naye imetoa msimamo wake, Waziri wa baraza la kimataifa wa serikali ya shirikisho ya Urusi Konstantin Kosaçev alisema tumejaribu kulitatua suala hili kwa njia za kidiplomasia imeshindikana kufikia muafaka,sasa tutabadili  njia za kulishughulikia suala hili. "Vile hatuafikiani katika suala hili, ambalo ilibidi tuafikiane basi na sisi tutafanya vilevile walivyofanya wao" alisema.

Kutokana na jasusi wa zamani wa Urusi Sergey Skripal pamoja na binti yake Yulia Skripal kulishwa sumu katika mji wa Salisbury mwezi machi mwaka huu, uliibuka mgogoro mkubwa kati ya mataifa haya mawili iliyosababisha serikali ya Uingereza kufukuza wanadiplomasia 23 wa Urusi ambayo nayo imeamua kujibu mapigo kwa kufukuza wanadiplomasia wa Uingreza nchini Urusi.Habari Zinazohusiana