7 wauawa na 154 kujirehuwa Ukanda wa Gaza

Raia 7 Wapalestina wauawa na wengine 154 kujeruhiwa kwa risasi za moto katika maandamano Ukanda wa Gaza

7 wauawa na 154 kujirehuwa Ukanda wa Gaza

Watu 7 wameuwa na wengine zaidi ya 154 kujeruhiwa katika mpaka wa Gaza uliofungwa baada askari wa Israel kuwafyatulia risasi wananchi wa Palestina waliokuwa wakiandamana.

Wapalestina tangu mwanzoni mwa mwaka 2018 wamekuwa wakiandamanaa kupinga kuzuiliwa kwao kurejea katika  makaazi yao.

Msemaji wa wizara ya afya ya Palestina Eshref El Kudra, katika taarifa yake ya maandishi alifahamisha kwamba  maeneo tofauti katika mpaka wa Gaza watu watano walijeruhiwa vibaya sana na wengine 154 kujeruhiwa kwa kupigwa risasi za moto kati ya watu hao 50 ni watoto na 10 ni wanawake

Katika habari nyingine waziri wa ulinzi wa Izrael Avigdor Liberman ameamrisha kusimamisha usambazaji wa nishati katika ukanda wa gaza.

Liberman alisema kama haya matukio yataendelea kutokea katika mpaka wa Gaza hawataruhusu nishati iingie eneo hilo.

Gazeti la Izrail la Haaretz wiki iliyopita liliripoti kuwa mkataba wa mradi wa umeme ambapo Katar ndio ingefadhili ununuaji wa nishati ulisainiwa.

Katika maelezo mengine yaliyotolewa na wizara ya afya ya Palestina " katika maeneo mbalimbali ya mpaka wa Gaza askari wa Izrail walifyatua risasi za moto na kuuwa watu 6".

Tangu tar 30 mwezi wa tatu mwaka huu Wapalestina wameandaa maandano ya amani yanayojulikana kama maandamano makubwa ya kurudi katika eneo lililoshikiwa na Waizrail katika mpaka wa Ukanda wa Gaza.

Askeri wa Izrael hupiga risasi za moto raia wa Palestina ambao wanaandamana kutaka eneo lao la ardhi lililokaliwa kimabavu na Izrael liachiwe pamoja na kudai vikwazo visivyokuwa vya haki walivyowekewa tangu mwaka 2006 viondolewa.

Tangu maandamano haya yaanze tar 30 mwezi wa tatu mpaka hivi sasa Wapalestina zaidi ya 200 wameuwa. 

 

 Habari Zinazohusiana