Rais Putin aahidi Kuisaidia Venezuela

Raisi Putin asema Urusi ipo tayari kuisaidia Venezuela iweze kujikwamua katika matatizo ya kiuchumi na kijamii yanayoikabili

Rais Putin aahidi Kuisaidia Venezuela

Rais wa taifala Urusi Vladmir Putin amesema wapo tayari kuisaidia Venenzuela ili iweze kujikwamua katika matatizo ya kiuchumi na kijamii yanaloikumba taifa hilo hivi sasa.

Wakati wa sherehe ya utambulisho wa balozi mpya wa Venezuela nchini Urusi, Rais Putin aligusia suala la Venezuela

Kiongozi huyo wa Urusi alisema,

"Uongozi wa Venezuela ni marafiki wakubwa wa taifa hili, tunawatakia jamii yote ya Wavenezuela wafikie mafanikio kiuchumi na kijamii na katika hili tupo tayari kutoa msaada wowote unaohitajika." alitumia maneno hayo Putin

Mazungumzo kati ya Urusi na Venezuela yataendelea alisema Putin, pia alisisitiza kuwa Moskow ipo tayari kusaidi katika miradi ya nishati, viwanda na maeneo mengine watayoamua kushirikiana.Habari Zinazohusiana