Mike Pence na FBI katika sakata la Jamal Khashoggi

Marekani ipo tayari kutuma wataalamu wa FBI kama Saudia wakitaka kuchunguza kizungumkuti cha Jamal Khashoggi

Mike Pence na FBI katika sakata la Jamal Khashoggi

Jamal Khashoggi , mwandishi wa habari ambae tarehe 2 mwezi wa kumi aliingia katika ubalozi mdogo wa Saudia, jijini İstanbul mpaka hii leo hajaonekana. Ni fumbo linalokosa jibu.

Makamu wa rais wa Marekani Mike Spence amesema kama Saudia wakitaka wao wako tayari kutuma wachunguzi wa shirika la uchunguzi la Marekani FBI kwenda nchini Uturuki kufanya uchunguzi.

Katika kipindi kimoja cha redio Pence amesema wako tayari kutoa chochote kinachohitajika kusaidia kupatşkana mwanahabari huyu.

Kama Saudı Arabia wakituomba tupo tayari kutuma wataalamu kutoka FBI kwenda Uturuki kufanya uchunguzi, alisema Pence.Habari Zinazohusiana