Malaria yazua hofu nchini Indonesia

vituo vingi vya afya viliangamizwa katika tetemeko la ardhi.

Malaria yazua hofu nchini Indonesia

Indonesia imetangaza dharura kutokana na kuzuka kwa malaria katika kisiwa cha Lombok Island, ambapo zaidi ya watu 560 wamepoteza maisha katika tetemeko la ardhi lililotokea mwezi uliopita.

Kulingana na ripoti za vyombo vya habari, ugonjwa wa malaria umekiandama kisiwa hicho ambapo watu wapatao 450,000 wasiokuwa na makazi walihamishiwa.

Kwa mujibu wa habari,vituo vingi vya afya viliangamizwa katika tetemeko la ardhi.

Hali hiyo imesababisha kuwa vigumu kwa wagonjwa kupewa matibabu muhimu.

Mpaka sasa watu zaidi ya 100 wameripotiwa kupatwa na malaria kali.

 Habari Zinazohusiana