Dhoruba laua watu 12 Ufilipino

Watu 12 wameripotiwa kupoteza maisha baada ya dhoruba kuikumba kaskazini mwa Ufilipino.

Dhoruba laua watu 12 Ufilipino

Watu 12 wameripotiwa kupoteza maisha baada ya dhoruba kuikumba kaskazini mwa Ufilipino.

Dhoruba Mangkhut limeipiga nchi hiyo masaa ya Jumamosi asubuhi.

Mshauri wa rais Rodrigo Duterte,Francis Tolentino amesema kuwa watu 12 wamefariki na wengine hawajulikani walipo kutokana na janga hilo.

Watu 87,000 wameyahama makazi yao.

Kulingana na vyombo vya habari nchini humo,Duterte atafika katika maeneo yaliyoathirika pale tu mamlaka katika uwanja wa ndege yatakapomtaarifu kuwa anaweza kusafiri.

Timu za uokozi zinaendelea na kazi yake.Habari Zinazohusiana