"Ununuzi wa F-400 ni uamuzi wa kitaifa"

Katibu  mkuu wa NATO  Jens Stoltenburg amesema kuwa ununuzi wa S-400 na Uturuki ni uamuzi uliochukuliwa na Uturuki yenyewe kama taifa.

"Ununuzi wa F-400 ni uamuzi wa kitaifa"

Katibu  mkuu wa NATO  Jens Stoltenburg amesema kuwa ununuzi wa S-400 na Uturuki ni uamuzi uliochukuliwa na Uturuki yenyewe kama taifa.

 Jens Stoltenburg amesema kuwa uamuzi huo umefanywa na Uturuki yenyewe kama mnunuzi na Urusi kama muuzaji.

Kumekuwa na malumbano kuhusu suala hilo na ni dhahiri kwamba Marekani haijafurahishwa na kitendo hicho.

Katibu huyo ameongeza kwa kusema kuwa suala muhimu kwa NATO ni kufanya kazi kwa ushirikiano.

Mnamo Desemba mwaka jana,Uturuki ilitangaza kununua makombora ya S-400 kutoka Urusi ambayo yatakuwa tayari 2020.

Baada ya Uturuki kutangaza hivyo,bunge la Marekani nalo lilichukua uamuzi wa kutoiuzia Uturuki ndege za  F-35 mwezi Juni mwaka huu.

 


Tagi: S-400 , Uturuki , NATO

Habari Zinazohusiana