Yusuf Nazik , muhusika wa shambulizi la Reyhanli Syria akamatwa

Muhisika mkuu wa shambulizi la Reyhanli Syria akamatwa baada ya kutafutwa  muda mrefu . Gaidi huyo amekamatwa na kukiri  uhalifu aliotenda

reyhanli saldiri.jpg

Muhisika mkuu wa shambulizi la Reyhanli Syria akamatwa baada ya kutafutwa  muda mrefu . Gaidi huyo amekamatwa na kukiri  uhalifu aliotenda. 

Yusuf Nazik  alikuwa akitafutwa na wizara ya mambo ya ndani ya  Uturuki baada ya kuendesha mauaji.

Shirika la upelelezi la Uturuki limemkamata gaidi huyo nchini Syria na kumsafirisha nchini Uturuki.

Yusuf Nazik  ni muhusika mkuu wa shambulizi la Reyhanli  Kusini-Mashariki mwa Uturuki . Shambulizi hilo  lilisababisha vifo vya watu 53 mwaka 2013.

Kulingana na taarifa zilizotolewa  Jumatano na vyombo vya usalama, Yusuf  Nazik amelkamatwa Lattakia nchini Syria  katika operesheni  kabemba aliokuwa ikiendelea.

Gaidi huyo amekiri kuhusika na shambulizi hilo  ambapo amesema kuwa alikuwa akitekeleza  wajibu wake katika  vikosi vya ujasusi vya Syria.

Mei 11 mwaka 2013,  Reyhanli ilishambuliwa kwa mabomu mawili na kusababisha vifo vya watu 53.

 Habari Zinazohusiana