Uturuki yalaani uamuzi wa Marekani kufunga uakilishi wa Mamlaka ya wapalestina Washington

Uturuki kupitia msemaji wa wizara ya mambo ya nje imelaani vikali uamuzi wa Marekani kufunga uakilishi wa mamlaka ya wapalestina mjini Washington

Uturuki yalaani uamuzi wa Marekani kufunga uakilishi wa Mamlaka ya wapalestina Washington

Uturuki kupitia msemaji wa wizara ya mambo ya nje Hami Aksoy  imelaani vikali uamuzi wa Marekani kufunga uakilishi wa mamlaka ya wapalestina mjini Washington.

Kwa mujibu wa Uturuki, uamuzi huo wa kufunga uakilishi wa Mamlaka  ya wapalestina hauna malengo yeyote zaidi ya  kuunga mkono  wale ambao wanataka kutupilia mbali   suluhu la  mzozo wa Mashariki ya Kati.

Suluhu la mataifa mawili ni mada ambayo inatakiwa kuzungumziwa ili kutatau mzozo  kati ya Israel na Palestina.

Hami Aksoy  amesema kuwa  Marekani kuchukuwa uamuzi wa kufunga  uakilishi wa Mamlaka ya wapalestina mjini Washington , ni wazi kuwa  Marekani inaegemea upande mmoja.

 Habari Zinazohusiana