Erdoğan: Mashambulizi  ya jeshi la Syria Idlib yataathiri usalama Ulaya

Rais wa Uturuki Recep Tayyığp Erdoğan asema kuwa mashambulizi ya jeshi la Assad Idlib  yataathiri usalama  barani Ulaya

Erdoğan: Mashambulizi  ya jeshi la Syria Idlib yataathiri usalama Ulaya

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan  asema kuwa  mashambulizi ya jeshi la Syria İdlib yatakuwa athari kubwa ya kiusalama  barani Ulaya.

Kwa mujibu wa rais Erdoğan , malengo ya mashambulizi ya  jeshi la Syria Idlib  sio kukabiliana na ugaidi bali  kutaka kudhoofisha nguvu upinzani.

Katika makala ilioandikwa katika jarida la Marekani la Wall Street Journal,  rais Erdoğan amesema kuwa jumuiya ya kimataifa  inatakiwa  kufahamu kuwa  mashambulizi hayo yatakuwa na athari kubwa na kuwatia raia katika madhila.

Rais wa Uturuki ameendelea kusema kwamba  Uturuki haitowaacha raia wa Syria  chini ya unyama wa Assad.

Iwapo Ulaya na Marekani haizitochukuwa  hatua  basi ni wasyria watakaoathirika na tatizo hilo  litakuwa la ulimwenguni mzima.  Uturuki imekwishafanya  kilichowezekana na kupokea wa kimbizi zaidi ya milioni 3,5 kutoka Syria.

Rais Erdoğan amezungumzia pia  kuhusu mashambulizi ya kundi la wanamgambo wa Daesh na kundi la kigaidi la PKK, gharama ya  kuhudumia wakimbizi na mahataji mengine .

Rais wa Uturuki amezungumzia pia kuhusu silaha za kemikali kwa kusema kuwa sio tu kukemea silaha hizo kwa kuwa silaha zote zinazotumiwa Syria zinasababisha maafa jambo muhimu ni kupatia suluhu mzozo unaoendelea nchini humo.Habari Zinazohusiana