Gari la kupaa nchini Japan
Mradi wa kutengeneza gari lenye uwezo wa kupaa umeanza rasmi nchini Japan.

Mradi wa kutengeneza gari lenye uwezo wa kupaa umeanza rasmi nchini Japan.
Kulingana na vyombo vya habari vya Japan kampuni 20 zinashirikiana katika kuhakikisha mradi huo unafanikiwa.
Uber, Japan Airlines, Airbus, Boeing, NEC, Toyota, ANA na Yamato ni kati ka kampuni zinazohusika na utengenezaji wa gari hilo la kipekee.
Wizara ya uchumi,biashara na viwanda nchini Japan imesema kuwa mradi huo utatumia bajeti ya $ 40.4 milioni.
Gari la kupaa linatajia kukamilika ifikapo 2020.