Wagonjwa wataabika Gaza

Wagonjwa wa saratani wanazidi kuhangaika baada ya dawa za kuutibu ugonjwa huo kumalizika Gaza.

Wagonjwa wataabika Gaza

Wagonjwa wa saratani wanazidi kuhangaika baada ya dawa za kuutibu ugonjwa huo kumalizika Gaza.

Msemaji wa wizara  ya afya Al Kudra amesema kuwa kuisha kwa dawa hizo hospitalini kumesababisha kusitishwa kwa matibabu kwa wagonjwa wa saratani.

Kudra amesisitiza kuwa maisha ya wananchi wengi yapo hatarini kama dawa hizo hazitapatikana.

Hospitali ya viongozi wa Hamas ndio hospitali pekee yenye kitengo cha kutoa matibabu kwa wagonjwa wa saratani Gaza.

Mashambulizi ambayo yamekuwa yakiendelea Gaza katika miaka ya hivi karibuni yamepelekea matatizo mengi ikiwemo uhaba wa huduma za afya.Habari Zinazohusiana