Iraq yasitisha ushirikiano wake wa kibiashara na Iran

Iraq imeacha kufanya biashara na Iran baada ya Marekani kuiwekea vikwazo Iran.

Iraq yasitisha ushirikiano wake wa kibiashara na Iran

Iraq yasitisha ushirikiano wake wa kibiashara na Iran baada ya Marekani kuiwekea vikwazo Iran.

Benki kuu ya Iraq imetoa onyo kwa benki zote kuwa biashara na Iran imepigwa marufuku.

Msemaji wa serikali ya Iraq Saad al-Hadith amesema kuwa itakuwa vigumu kwa nchi hizo mbili kuendeleza mahusiano ya kibiashara baada ya vikwazo  vilivyowekwa na Marekani dhidi ya Iran.

"Tutatumia mbinu mpya kupunguza athari zinazoletwa na vikwazo hivyo katika biashara",alisema Saad.

Mnamo Jumanne Marekani iliiwekea vikwazo Iran ikilenga hasa sekta ya benki.


Tagi: biashara , Iraq , Iran

Habari Zinazohusiana