Erdoğan : "Uturuki ipo tayari kutumia sarafu za ndani katika biashara"

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan asema kuwa Uturuki ipo tayari kuanza kufanya biashara kwa kutumia sarafu za ndani badala ya kumia sarafu ya Marekani

Erdoğan : "Uturuki ipo tayari kutumia sarafu za ndani katika biashara"

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan asema kuwa Uturuki ipo tayari kuanza kufanya biashara kwa kutumia sarafu za ndani badala ya kumia sarafu ya Marekani.

Hayo rais Erdoğan amezungumza katika ziara yake mkoani Rize Jumamosi Kaskazini-Mashariki mwa Uturuki.

Uturuki kwa ushirikiano na mataifa ambayo yanashirikiana kwa kiasi kikubwa katika biashara kama China, Urusi, Iran na Ukraini ipo katika mikakati ya kutumia sarafu za ndani badala ya sarafu ya Marekani dola katika biashara.

Rais Erdoğan amezungumzia  kodi ya ziada iliongezwa kama kikwazo kwa Uturuki na rais wa Marekani Donald Trump.

Rais wa Uturuki alitembelea pia eneo ambalo lilikumbwa na mafuriko mkoani Ordu Jumatano na kusababisha uharibifu .

Mgogoro katika ya Marekani na Uturuki umeibuka  tangu Marekani kutangaza kuwawekea vikwazo waziri wa mambo ya ndani wa Uturuki Süleyman Soylu na waziri wa  sheria Abdulhamit Gül  kufuatia tuhuma zinazomkabili mchungaji Andrew Brunson ambae alikamatwa akituhumiwa kushirikiano na  kundi la kigaidi.

 

 Habari Zinazohusiana