Ujumbe kutoka kwa rais wa Iran kwa rais wa Uturuki kuhusu vikwazo vya Marekani

Rais wa Iran Hassan Rouhani amtumia ujumbe rais wa Uturuki  kuhusu vikwazo vilivyowekwa na rais wa Marekani dhidi ya Uturuki

erdogan rize.jpg
ruhani.jpg

 

Rais wa Iran amtumia ujumbe rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan  kuhusu vikwazo vilivyowekwa na rais wa Marekani Donald Trump dhidi ya Uturuki .

Katika ujumbe huo rais wa Iran amemfahamisha rais wa Uturuki kuwa  Marekani itajuta  kwa uamuzi iliochukuwa dhidi ya Uturuki.

Mjumbe maalum wa rais Rouhani , Mahmud Vaizi amefikisha ujumbe kwa rais wa Uturuki kutoka kwa Rouhani. Ujumbe huo unafahamisha kuwa Marekani itajuta kwa uamuzi uliochukuliwa na rais Trump dhidi ya Uturuki.

Kulingana na taarifa zilizotolewa na shirika la habari la IRNA, mkutano kati ya mjumbe huyo kutoka Iran na rais Erdoğan walizungumzia  kuhusu makubaliano ya nyuklia ya Iran ya mwaka 2015 na vikwazo vya Marekani dhidi ya Uturuki.

Mjumbe huyo ameendelea kufahamisha kuwa Iran itaendelea kukabiliana na Marekani hadi itakapo juta kwa uamuzi wake iliochukuwa.

Kwa upande wake rais Erdoğan amesema kuwa ujumbe wa rais Rouhani umepoklewa kwa mikono miwili  na Uturuki itaendelea kushirikiana na Iran  na kuondoa  vizuizi katika ushirikiano uliopo baina ya Uturuki na Iran.

Katika ziara yake hiyo nchini Uturuki, Vaizi alizungumza pia waziri wa mbo ya nje wa Uturuki Mevlüt Çavuşoğlu.

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki amesema kuwa Uturuki haitofuata vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran.

 Habari Zinazohusiana