Rais Erdoğan kufanya ziara ra nchini Ujerumani

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan atarajiwa kufanya ziara nchini Ujerumani Septemba

Rais Erdoğan kufanya ziara ra nchini Ujerumani

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan atarajiwa kufanya ziara rasmi nchini Ujerumani ifikapo mwezi Septemba.

Ziara hiyo  ya rais Erdoğan  nchini Ujerumani itachukuwa muda wa siku  mbili kuanzia Septemba 28 hadi Septemba 29.

Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier  atampokea rais  Erdoğan  kama ilivyofahamishwa na vyanzo vya habari nchini Ujerumani.

Katika ziara hiyo rais wa Uturuki atazungumza pia na kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel. Taarifa  kuhusu ziara ya rais Erdoğan nchini Ujerumani imetolewa na jarida la DPA.

Mwishoni mwa Julai ofisi za rais wa Ujerumani zilifahamisha kuwa rais wa Uturuki atafanya ziara nchini Ujerumani bila ya kufahamisha siku. 

Ziara ya mwisho ya rais wa Uturuki mjini Berlin ilifanyika Februari  mwaka 2014.Habari Zinazohusiana