Rais Putin azungumza kwa njia ya simu na rais wa Uturuki kuhusu ushirikiano

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan azungumza kwa njia ya simu na rais wa Urusi Vladimir Putin kuhusu ushirikiano kati  ya Uturuki na Urusi

erdoğan telefon.jpg

 

Rais wa Uturuki azungumza kwa njia ya simu na rais wa Urusi Vladimir Putin  kuhusu ushirikiano baina ya Uturuki na Urusi . 

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na kitengo cha upashaji habari ikulu mjini Ankara, katika mazungumzo hayo kati ya rais Erdoğan na rais Putin kulizungumziwa ushirikiano katika sekta ya biashara, uchumi, ulinzi , nishati , mzozo wa Syria na  hatua iliofikiwa katika mazungumzo ya  amani kuhusu Syria mjini Astana.

 Viongozi hao wamepongeza  hatua iliopigwa katika  ushirikiano  baina ya Uturuki na Urusi.

 Habari Zinazohusiana