Myanmar na uchunguzi wa Mahakama ya kimataifa ya uhalifu

Myanmar yakemea   pendekezo la Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita  ICC

Myanmar na uchunguzi wa  Mahakama ya kimataifa ya uhalifu

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC imefahamisha kuwa inataraji kuanza uchunguzi kuhusu mauaji  na uhalifu vilivyoendeshwa dhidi ya waislamu wa jamii ya Rohingya.

Waislmu jamii ya Rohingya Myanmar  zaidi ya 700 000 walilazinika kuhama  makaazi yao wakihofia maisha yao  kutokana na mashambulizi dhidi yao Rakhine. 

Rohingya hao walikimbilia nchini Bangladesh kutafuta hifadhi.

Taarifa ilizotolewa na  kwa ushirikiano na wizara ya mambo ya nje na  wizara inayohusika na  uongozi wa rais chini ya  Aung Sn Suu Chii imefahamisha kuwa mahakama ya kimataifa nchini Uholanzi haina haki ya  kuihukumu Myanmar kwa kuwa Myanmar sio mwanachama wa mahakama hiyo.

Mahakam ya ICC iliiomba Myanmar kutoa jibu la ombi la kuendesha uchunguzi  kuhusu madhila yaliowakumba waislamu wa jamii ya Rohingya  hadi Julai 27 mwaka 2018.

 

 


Tagi: Rohingya , ICC , Myanmar

Habari Zinazohusiana