Ahmedinejad amtolea wito rais Rouhani kujiuzulu

Rais wa zamani wa Iran Mahmud amtolea wito rais Hassan Rouhani kujiuzulu

Ahmedinejad amtolea wito rais Rouhani kujiuzulu


Rais wa zamani wa Iran Ahmednejad amtolea wito rais Hassan Rouhani kujiuzulu  nchini humo. 

Rais huyo wa zamani  nchini Iran amesema kuwa  wito huo ameutoa kufuatia hali mbayo inaendelea nchini Iran.

Mahmud Ahmednejad ametoa ujumbe katika  ukurasa wake  mmoja kati ya kurasa zake katika mitandao ya kijamii  akifahamisha kuwa  raia nchini Iran  hawaridhishwi na hali inayoendelea nchini humo.  

Katika ujumbe wake Mahmud Ahmednejad ameendelea kuzungumzia pia kuhusu uchumi ambao unaonekana kuzidi kudidimia na raia nchini humo wamepoteza matumaini na utawala.

Kutokana na hali hiyo Mahmud Ahmednejad ametoa  wito kwa Rouhani kujiuzulu.Habari Zinazohusiana